Ray Vanny “Unaibiwa” Lyrics

download

Verse 1
Usidate na njonjo za mapenzi
vicheko bandia usoni kudeka
Kumbe ana pretend
Maufundi toka tanga na zenji
Vionjo mitego unase
Ashike pochi umwage chenji
Anakuchanganya kiunoni shanga
Marashi kama uko peponi
Mtoto sauti kinanda ya kumtoa
Chatu pangoni
Ukishatafuna karanga
Hutaki hata aende sokoni
Anakuchuna mafaranga
Unabaki na vummbi mfukoni
Ukiwa na pesa utasifiwa kitambi
Babe me I like that
Na kukupamba kwenye simu
Video snapchat
Kumbe hana mana hadi mangi
Anamwita sweetheart
Kisa anakesha gym kutafuta six packs
Chorus
Unaibiwa unaibiwa
Unaibiwa unaibiwa
Unaibiwa unaibiwa
Verse 2
Kuna akina rose visosa
Wale wapenda Verossa
Ukipita na shati na moka
Lazima watashoboka
Wakiomba lift ogopa
Viguu dashbodi vishoka
Mchunguze cheni ghoroka
Nywele na pochi kakopa
Eeeeh usije kuyavamia
Yasije yakakutesa
Hawachelewagi kukimbia
Kuna wenzako wanalia
Walidhani mapenzi pesa
Kwenye suruali vibamia
Hata ukimuonga ferrari
Hatokuona lijali
Wakati chumbani we beki ukifunga
Goli moja tu chali
Atakamatwa na mangangali
Vijana machachali
Hawachagui sehemu ya vita
Uvunguni na juu ya dali
Ukiwa na pesa utasifiwa kitambi
Babe me I like that
Na kukupamba kwenye simu
Video snapchat
Kumbe hana mana hadi mangi
Anamwita sweetheart
Kisa anakesha gym kutafuta six packs
Chorus
Unaibiwa unaibiwa
Unaibiwa unaibiwa
Unaibiwa unaibiwa
Verse 3
Unadhani ni wa peke yako
Kumbe wengine wameshaweka kambi
Kakupendea macho
Wapo wengine kawapendea rangi
Yeye ni Gari la dampo
Hachagui taka dereva mpe ganji
Wa kubadili sample
Akila mihogo caroti hazipandi
Chorus
Unaibiwa unaibiwa
Unaibiwa unaibiwa
Unaibiwa unaibiwa

download Nyimbo mpya