Ray Vanny “Siri” (ft Niki Wa Pili) | Lyrics

download

Nimeanza safari ya mapenzi na wewe
Usiikatishe eeh Mungu mwema Baba
Mbali atufikishe eeh
Mimi ni Binadamu nakosea
Nikiteleza usiuzunike eeh
Milele mwanadada nikifa unizike
Kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu
Natamka ni wewe
Taswira pekee kwenye ndoto zangu
Mama
Nifariji pekee nikiwa na chozi langu
Mama Ni wewe
Imenishinda siri kifuani mwangu
Aaah

Nikupeleke nyumbani kwetu
Sheri eeeh
Ukawajue na ndugu zangu
Mama aah
Unipeleke nyumbani kwenu
Bibi wewe Nikawaone
Shemeji zangu mamaa

Ooh mama Roda
Oooh mama Roro
ooh mama Roda

Mama nipe utamu kabla hujatamka
Usingizi sicum mpaka tukiamka
Ni siri hizi Kakonko
Twende kamara Kibilizi
Mapaja yake utamu michirizi
Michepuko imenuna imezira siri siri
Na wewe ni kachumbari mayonnize pilipili
Pili pili manga tunakili kili wanga
Kilimanjaro nyumbani kwetu Kisimiri
mwanga
Simama Nikki simama wima
Siri ni kilele nikufikishe kwa kina
Umebeba beba mkungu wa Muleba
Uchungu kama kwao wakajifungue leba
Umebeba beba mkungu wa Muleba
Uchungu kama kwao wakajifungue leba

Oh mama Roda
Mama Roro kwako sijiwezi
Oh Mama Roro sitoficha mdudu mapenzi
Oh Mama Roda
Mama Roro kwako sijiwezi
Oh Mama Roro Mama Roro ooh

Kwenye ka moyo mimi sina siri
Acha nikutaje ka jina siri
Wajue wenye fitina siri
Jembe nipo nalima Siri
Basi nawe usifiche mama (Siri)
Sema watupishe na (Siri)
Vichefuchefu watapishe ma (Siri)
Penzi letu lisishe ma (siri)
Mimi na wewe
Owe owe oh
owe owe oha
Owe owe oh
Owe owe oha

Siri ya nini (owe owe ooh)
Nini maana yake (owe owe oha)
Siri ya nini (owe owe ooh)
Nini hasara zake (owe owe oha)

download Nyimbo mpya