#SeduceMe : Namjua Mfalme Mmoja Tu,Ali Kiba- Christina Shusho Akiri

download

Baada ya Diamond Platinumz kuanzisha ama kufufua bifu kati yake na Ali Kiba,kumekuwa na hisia mseto kutoka kambi zote mbili za wasanii hao tajika.

Msanii wa nyimbo za injili Christina Shusho pia ameingilia uhasama huo ambao unatokota kwa kasi sana.

Christina Shusho anadai wimbo mpya wa Ali Kiba ni mzuri na anaweza keti na familia kutazama maana picha zilizomo ndani si za aibu.

“Leo unaeza kuta mtu kaitwa kanisani aongoze wimbo wa sifa halafu akalianzisha seduce me….eeh jamani Kiba we noma. – Wimbo ni mzuri sana Professionally in Boss ruge ‘s voice. – Hauna picha za aibu , naeza watch na familia, though sijui maana ya SEDUCE ME. #teamkigoma #wamanyema oyeeeee LAST @OFFICIALALIKIBA BASI SIKU NYINGINE TUTEMBELEE KANISANI. UKIWA MFALME HUCHAGUI DINI WOTE WAKO.” – Christina Shusho

Vile vile Shusho amemwalika Ali Kiba Kanisani kuwaimbia.

Vibe Download Button

Leave a Reply