Msanii Madini Classic Anasaka Kiki Au Ni Povu Tu ?

download

Mr. Kalongolongo au ukipenda Madini Classic amezua gumzo mtandaoni baada ya kufufua bifu kati ya Otile Brown na Bahati. Ikumbukwe kuwa Bahati na Otile Brown walitofautiana mwaka uliopita. Hii ni baada ya Otile Brown kudai kuwa Bahati alifeli kwa mashairi kwenye wimbo wake waliofanya na Eddy Kenzo,Barua Kwa Mama.

Sasa Msanii Chipukizi ameamsha bifu hilo. Kiaje?

image
Otile Brown Na Shetta

Msanii huyo amedai kuwa wimbo mpya wa Otile Brown,Tamu Sana aliomshirikisha Shetta kuwa sio mtamu.

” Jamanie muda mwingine sisi wasanii tunapoongea kwenye media Mara nyingi mmesikia tukisema kwamba tushikane mikono tupeane support kwa wenzetu ili tufike mbali, lakini nilishangaa sana kipindi flani msanii flani akisema kwamba bahati amewaste collabo na kudai kua eti bahati hajui kuandika na akaona bora angemwandikia sawa. Haya maneno aliziandika hadharani kwenye social media platformz zake watu wengine walimshangilia sana hehe!!! nilisikia ila nikasema freshy pengine yeye yuajua sana lakini sasa mbona kama kwangu mimi nahisi huu wimbo nimeuskiza leo unaitwa #TAMUSANA Ni yake na Shetta au? maanake nahisi Shetta kaifanyia haki sana ile biti zaidi ya mhusika mkuu……Muda mwingine unapodharau nyuma na kuona mapungufu ya wenzako kua makini huenda mbele kukawa na giza, najua pengine wewe ni shabiki yake utantolea povu ila dah ukweli tuseme Bahati angefanya Vizuri na Shetta na wimbo wenyewe ungekua TAMUSANA cha msingi tusapotiane tukosoane kwa upendo na heshima ili wanaotusoma kama vile role models wao waige tabia njema kutoka kwetu Ila huo wimbo sio tamu .”

image
Msanii Madini

MADINI ambaye alitoka kwa mara ya kwanza baada ya kufanya cover ya wimbo wa RAYVANNY ‘KWETU.

download Nyimbo mpya