Mhusika Mkuu Kwa Kifo Cha Mowzey Radio Akamatwa!

Mtuhumiwa wa kifo cha Mowzey Radio mikononi mwa Polisi.

Mtuhumiwa namba moja ambaye anahusishwa na kifo cha msanii muziki nchini Uganda, Mowzey Radio amekamtwa na Jeshi la Polisi nchini humo.

Kijana Wamala Godfrey mwenye umri wa miaka 28 ndiye alikuwa akisakwa na polisi kama mtuhumiwa mkuu mara baada ya mmiliki wa bar, Egesa George na Meneja wake kilipotokea kifo cha Radio kushikiliwa na Polisi.

Mwimbaji Mowzey Radio alifariki dunia Februari Mosi mwaka huu kutokana na majeraha ambayo aliyapata kichwani kufuatia ugomvi katika bar hiyo.

Kamanda wa Polisi Kampala, CP. Frank Mwesigwa amethibitisha kushikiliwa kwa Wamala Godfrey na kueleza kuwa kwa sasa wanaandaa majalada ili kuweza kumfikisha mahakamani.