Entertainment Gossip

Janga Kuu !!! Ben Pol Amtoka Mpenziwe

download

Muigizaji #Ebitoke amefunguka na kusema kuwa msanii Ben Pol amemuacha na yeye ameamua kumuacha pia aendelee na maisha yake kwani amejigundua ni kama alikuwa analazimisha mapenzi kwa Ben Pol na mwisho wa siku kujikuta anakosa furaha na amani.

Ebitoke alisema hayo alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha Papaso kwenye Television ya Taifa na kusema baada ya kukubaliana na hali hiyo saizi amejikuta ana furaha na amani ndani yake kwa kuwa hakuna kitu kinachompa mawazo tena.

“Unajua mapenzi ni hisia na yanahitaji sana furaha sasa mimi niligundua namlazimisha Ben Pol hivyo nikaamua kumuacha aendelee na maisha yake ya kawaida, yeye ndiye aliyeanza kuniacha kwani muda mwingi alikuwa anasema yupo busy na mimi nikasema basi ngoja nifanye vitu vyangu maana mwenyewe pia na ndoto zangu nyingi tu, japo nilikuwa naumia lakini saizi nina furaha na maisha haya mapya” alisema Ebitoke.

#mambomseto

download Nyimbo mpya

Leave a Reply