[Verse 1: Mbosso]
Yale yale ya ujana maji ya moto
Nikaukurupukiaa
Leo hii wawili watoto
Wanaiangaliaa
Napambana sana na Changamoto
Kuwafutiaa
Nikikosa mzazi mwenzangu
anakuja Moto
Matusi Kunshushiaa
Natumia nguvu Kutafuuta
Jasho laloesha shatii
Chini nikiziba ufa
Juu linaanguka bati
Zile ng’ong’o kwa ndugu jama
zishaishaga mazima (mie)
Miondoondo mlezi wa wana
lakini zali sinaa (miee)
[Bridge :Mbosso]
Ama sauti yangu kwa mungu baba (haisikiki)
Tuseme dua zangu mbingu ya saba (hazifiki yoyo)
[Chorus]
Futa chozi futa (husiulize nalia nini)
Futa chozi futa (naisi riziki yangu imepigwa pini)
Futa chozi futa (iyeee lele lelile)
Futa chozi futa (mungu baba nione)
(Verse 2: Bahati)
Nikiwa kazini akili zote zipo nyumbani
Nikiwa nyumbani wakusalishe sina amani
Nakazana sana Kimziki
Kweli napambana Kubahatisha riziki
Wanaomba mabaya na roho za choyo
Na ndugu zangu wakiwemo
Napata fupa mi Kibogoyo
Mungu ameninyima meno
Nikitazama watoto wangu
Nje ya ndoa wamezaliwa
kwenye imani ya dini yangu
wanasema nishakosea
[Bridge : Bahati]
Ama sauti yangu kwa mungu baba (eeh)
Tuseme dua zangu mbingu ya saba (hazifiki baba eh)
[Chorus]
Futa chozi futa (kuna muda naishiwa nguvu)
Futa chozi futa (elimu sina kichwa mbumbuu)
Futa chozi futa (naganga ganga njaa)
Futa chozi futa (eh mungu wangu lingi langu fungu).