Lyrics | Diamond Platnumz – Sikomi | Lyrics
Verse 1
Wanasema mapenzi safari unavyopita
Ndo jinsi unajongea
Ila niendapo ni mbali sijui ka
Ntafika sababu natembea
Niliposikia habari yakisifika
Nkakesha najongea ah
Akabariki Jalali nami nikawika
Muziki nikauotea
Ile pru mpaka maka
Nikandandiaga Bongo Movie
Kumbe mapenzi hayataki haraka
Ni kama tango natia tu chumvi
Mwenzenu nkaoza haswa
Nakujitia kitandani mjuzi
Eti nataka fukuza paka badala
Ya mbwa nikafuga mbuzi
Wivu ukanifanya nikagombana na marafiki
Ugomvi na mama angu akiniambia
Siambiliki
Moyo unaniambia Nasibu sasa mapenzi basi
Ila nangangania najaribu kuipinga nafsi
Esma ananiambia mdogo wangu
Mapenzi basii
Ila nangangania nikiumizwa na huyu
Kesho nina mwingine
Chorus
Oh Mbona sikomi sikomi sikomi
Licha ya mateso haya
Najiuliza oh sikomi oh sikomi Mondi
Sikomii Mola Jalali sikomi
Licha ya mateso haya
Verse 2
Alonifanyia wa central haki ya mungu
Siyawezi sema, Ila nimejifunza kesho
Siwaamini wacheza sinema
Moyo waliupatia mateso
Siwezi meza siwezi tema
Ndo maana sikushangaa ile ghafla
Toka ccm kwenda chadema
Wanasema kitanda ukitandika sharti ukilalie
Nikajitia ukamanda yatakwisha wacha
nivumilie
Kila kiza kikitanda ndo
Visa machozi mimi nilie
Penzi akatia parapanda
Kuwaita waje washambulie
Acha na Penny wa hidari
Niliemuongaga gari
Aliponiambia ana mimba mwisho wa siku
Akaichomoa chari
Mola akantunuku Zari
Akanzalia dume na mwari
Nilivyomjinga nkacheat
Aibu mpaka kwa vyombo vya habari
Moyo unaniambia Nasibu sasa mapenzi basi
Ila nangangania najaribu kuipinga nafsi
Lizer ananiambia Simba
Mapenzi basii
Ila nangangania nikiumizwa na huyu
Kesho nina mwingine
Chorus
Oh Mbona sikomi sikomi sikomi
Licha ya mateso haya
Najiuliza oh sikomi oh sikomi Mondi
Sikomii Mola Jalali sikomi
Licha ya mateso haya