Gossip

Muuzaji Ashambuliwa Kwa Kuuza Nyama Ya Paka

download

Kwa kawaida tumeziona habari nyingi za watu kufumaniwa wakiuza nyama ya punda au kumchinja punda.Hizi kwetu si habari ngeni kamwe.

Leo muuza mshikaki mmoja kakutwa wazi wazi akiuza nyama ya paka.Hii ni habari tuliyoipata kwa mujibu wa Umbea wa Tanzania Breaking News.

Muuza mishikaki mmoja maarufu katika kituo cha daladala cha Tegeta karibu kabisa na Pamba KALI jijini Dar es Salaam maarufu kwa jina la Said Mishikaki, amekamatwa na kupigwa na wananchi kwa tuhuma za kuuza mishikaki ya nyama ya paka. Said alikamatwa jana asubuhi baada ya taarifa kusambaa katika eneo hilo zikimtuhumu kwamba amekuwa na kawaida kuuza mishikaki ya nyama ya paka. Wateja wake wengi wakiwa ni boda boda na wana michezo wa Gym ya jirani iliyofunguliwa hivi karibuni.

Taarifa zilizopatikana kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, baada ya taarifa hizo kuenea, wananchi walilazimika kumtafuta muuza mishikaki huyo ili wamchukulie hatua. Baada ya kumsaka kwa dakika kadhaa, hatimaye walifanikiwa kumkamata na kumkuta akiwa na paka mmoja aliyekuwa amemchinja na kumuweka kwenye ndoo.

Wananchi wa maeneo ya tegeta kibaoni, kibo complex, na jirani na duka la Pamba kali mnashauriwa kujiepusha sana kula nyama za mishikaki na hasa wale wana mazoezi wa ile gym maana ndo wateja wake wakubwa na wala mishikaki kwa wingi. Pambaneni na hali zenu

download Nyimbo mpya

Leave a Reply