Mimi ni binti ninayefanya kazi kwenye Benki moja hapa Dar es Salaam.
Wakati natafuta kazi nilipewa mawasiliano ya huyu boss wangu hapa ambae baada ya kujitambulisha alinitaka. Kufika ili tuonane lakini baada ya mambo ya kazi kumalizika alinitongoza na kwakua ni boss halafu ni mzuri nilimkubalia na kujirusha nae mara kadhaa kabla ya kugundua kua ana mke na watoto wawili.
Nilimuuliza na akakubali kuwa ni ukweli. nikaona bora niendelee na maisha kwakua niligundua hakua na future nami.
Sasa nimepata mtu ambae anataka kunioa. Huyu boss wangu ameingia wivu ananiambia nichague kazi au huyo mwanaume, yani sijui nafanyaje sasa. Naomba mnishauri kipi nifanye kuondokana na hili tatizo?