Sababu Ya Ben Pol Kutoa Album Kimya Kimya

download

Msanii tajika wa Tanzania,Ben Pol Atoa Sababu Ya Kutoa Album Kimya kimya .

Msanii Ben Pol ametoa sababu ya kutoa album yake kimya kimya bila promo yoyote na kusema kwamba amefanya hivyo ili kuipa nafasi kazi yake mpya aliyofanya na msanii Chidinma kutoka Nigeria inayoitwa ‘Kidume’. Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Ben Pol amesema ameamua kufanya hivyo ili watu wasifikirie kuhusu album tu na waipe nafasi kubwa zaidi ‘kidume’, ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki, lakini hata hivyo atatoa taarifa namna gani mashabiki wake wanaweza kuipata albam yake mpya. “Kwa sababu nilitaka focus zaidi iwe kwenye wimbo mpya Kidume, halafu kuanzia wiki ijayo nitaanza kuongelea album na sehemu inakopatikana”, alisema Ben Pol. Album hiyo imebeba nyimbo 15 ambazo zilishatoka miaka ya nyuma na kufanya vizuri, imetoka kipindi ambacho watu walikuwa na kiu na Albam mpya ya Ben Pol ambayo alishawahi kuwaambia mashabiki kwamba atatoa albam mpya atakayoipa jina la mtoto wake, lakini imekuwa tofauti na kutoa albam yenye mjumuiko wa kazi zake za awali na mpya. – 57

Vibe Download Button

Leave a Reply