J DEE: BAADA YA MIMI NI VANESSA MDEE
Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Lady Jay Dee, amemtaja msanii Vanessa Mdee kuwa ndiye anayeweza kuwa mrithi wake endapo yeye atafutika katika ulingo wa bongo fleva.
Mkali huyo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘I miss you’, amesema anamkubali kazi za Vanessa, na kwamba anamuona ndiye msanii pekee mwenye utulivu, mipango na uwezo wa kuendelea kunyakua tuzo nyingi nje ya Tanzania.
Katika hatua nyingine mkali huyo wa hits kadhaa kama vile Ndindindi, Rosella, Sawa na wao n.k, ni kama amemrejesha kwenye game msanii Domokaya ambaye amepotea kwa muda mrefu kwenye anga ya muziki.
Domokaya aliyetamba miaka ya nyuma akiwa na Man Dojo, ameshiriki kwenye kuiandika ngoma hiyo ya Lady Jay Dee.
Je, wewe unaonaje, Vanessa ana uwezo wa kuwa kama Jay Dee?