Harmonize “Aiyola”
Intro
Wasafi Aiyo aiyola ieeh Aiyola mama aiyo aiyoola aieeh Mmh
Verse 1
Nilifundishwa na bibi kijijini jinsi ya kupenda Na mwanamke hapigwi Na ngumi ila upande wa khanga Tena mapenzi sio ligi nikakubali kushindwa Mi sikufunzwa biradhi Ushindani risasi kwa panga Mbona nilikuthamini Mengi nikakusevia Sikusema hadharani Wengi wakayasikia Si wakunipanda kichwani Hukumbuki tulipotokea Unaponishusha thamani Kipi nilichokosea Ingawa kidogo nilichopata Nikajinyima uridhike Ila hukujali ukanikatili moyo Majirani walinicheka Ulipoforce nipike Ah sio siri ilinivunja moyo Oh kisirani ugomvi bila chanjo Ni kweli upo moyoni Sina budi nilivue pendo Ingawa kishingo upande
Chorus
aiyo aiyola ieh sitoforce unipende aiyo aiyola ieh ooh kishingo upande mama aiyo aiyola ieh basi bora uendee aiyo aiyola ieh
Verse 2
Sitosema mapenzi basi Nimeumbwa nna moyo Moyo wenye matamanio Na unapenda pia Ila nitaijutia nafsi Nilikufanya chaguo Ah chaguo la moyo Kumbe ulipita njia Ah ah nilivowanyima ndugu Vi siri nikakutunzia Usijeleta vurugu Akili ukaitibua Najuta kujitia bubu Sitaki vya kusikia Kisa pendo unisulubu Mengi nishayafumbia Mbona nilikuthamini Mengi nikakusevia Sitosema hadharani Wengi wakayasikia Si wakunipanda kichwani Hukumbuki tulipotokea Unaponishusha thamani Kipi nilichokosea Oh kisirani ugomvi bila chanjo Ni kweli upo moyoni Sina budi nilivue pendo Ingawa kishingo upande
Chorus
Aiyo aiyola ieh Sitoforce unipende Aiyo aiyola ieh Ooh kishingo upande mama Aiyo aiyola ieh Basi bora uendee ma Aiyo aiyola ieh ingawa kishingo upande Aiyo aiyola ieh Sitoforce unipende Aiyo aiyola ieh Ooh kishingo upande mama Aiyo aiyola ieh Basi bora uendee Aiyo aiyola ieh Kishingo upande x2 Aaaaah