UKO WAPI LYRICS BY WILLIAM YILIMA

download

uko wapi eh mungu wangu ,
uko wapi njoo uniokoe x2
mawimbi yanataka kuniangamiza,
misukosuko yaniandama,
dhoruba na majaribu havikomi kwangu,

uko wapi fanya hima niokoe,x2
uko wapi eh bwana ,
uko wapi mbona ni kama umeniacha,
husifiche uso wako eh bwana,
husifiche uso nipone kwa rehema,
mwili huu wa nyama,
unachoka pekeangu sitaweza,x2
nimegumbikwa wimbi la huzuni na mawazo,
amani kwangu ni kama ndoto,
ole wangu nikifurahi siku moja,
siku sita nitalia wiki ipite,
mangumu yangu nikisimulia kwa ndugu zangu,
waniambia utajijua na mungu wako,
nikielezea mangumu yangu kwa wapendwa,
waniambia tumechoka kukufariji,
wakati mwingine natamani heri nife,
kuliko kuishi ninyanyasike hivi x2

uko wapi eh mungu wa elijah,
uko wapi eh mungu wa ibrahim,
uko wapi eh mungu wa isaka,
elshadai fanya hima uniokoe,
uko wapi eh bwana ,
uko wapi mbona ni kama umeniacha,

husifiche uso wako eh bwana,
husifiche uso nipone kwa rehema,
mwili huu wa nyama,
unachoka pekeangu sitaweza,x2
nina neno juu yako eh mpendwa,
husilie kwa mangumu uliyonayo,
husitazame jaribu ulilonalo,
inua macho msalabani umtazame yesu,
japo ndugu wakikutega na kukuacha,
yesu atakukumbatia,majaribu ipo siku
yatakoma,
utasahau shida zote ulizopata x2

If You are a Music Artist , Be it Upcoming or Famous And You wish To Drop Your Music For Fans To Access Online.

Whatsapp Us +254 720 350 193 for Deals.

download Nyimbo mpya