Nani Mkali , Rayvanny Ama Harmonize ?

download

Kambi kuu ya wasafi ipo motoni? Kisa ni utata kati ya wasani wawili walio na mukataba na Wasafi Records label chini ya uongozi wa msanii tajika nchini Tanzania  Diamond Platinumz.Je,nani mkali kati ya Rayvanny na Harmonize?

Harmonize alikuwa kipenzi cha wengi haswa mkubwa wake. Mtunzi mzuri na mwimbaji mzuri sana. Kila aimbapo waweza ukadhani ni Diamond wa pili,ila wanatofauti kisauti. Alitikisa anga na nyimbo zake zilizojaa hisia.Ayiola,Bado a Matatizo ziliteka anga za Afrika Mashariki.Wimbo matatizo ulimpa mafanikio makuu kote ukimwenguni . Hii ilipandisha hadhi yake na kujulikana kote kote.

Harmonize kwa kujituma kwake alishinda tuzo,hata kama hakujua kuboronga kilami.

Baada ya hela kuingia,Harmonize alijisatiri. Kuiga ikawa ndio mwonekanao wake. Alikopi kila kitu alichokifanya Mond. Kuanzia mavazi,kunyoa na pia tabia za kimapenzi. Ilikisiwa kuwa kwa wakati mmoja Harmonize alitoka kimapenzi na mpenzi wa zamani wa Mond.

Rayvanny

Kijana mtanatashi. Kiki ilimtoa vizuri. Rayvanny anauwezo mkubwa wa kuchana na pia kuimba.

Tangu apewe nafasi ya kuwa chini ya wasafi,hajawai angalia nyuma. Kila wakati utamkuta studioni akitunga nyimbo.

Wimbo salome ulitia kwenye ramani ya muziki na ukampa mafanikio mema licha ya utata uliouzingira wimbo huo.

Rayvanny alishinda tuzo hivi majuzi na kupokelewa vizuri nyumbani,Tanzania kutoka kwa uwanja wa ndege.

Bifu Baridi Kati Ya Harmonize na Rayvanny.

Kwa kiukweli nyota ya Harmonize imefunikwa na Rayvanny. Hivi karibuni huenda Harmonize akazimwa kabisa na tusimskie kabisa.

Rayvanny anajituma kabisa na utampata studioni muda mwingi.Hii imefanya yeye kudondosha nyimbo kiasi cha kuridhisha.Kwake Harmonize,hali ni tofauti kidogo. Licha ya kufanya kolabo na wasani wa kimataifa kama Mafikizolo bado hajatamba vizuri.

Anasa zinamzingira Harmonize na mapozi . Kwake Ravyanny ni mziki na familia.

Kwa hivi sasa Rayvanny ni mkali.
Tupia comment yako apo chini na kisha share .

Vibe Download Button