Baada ya kusikia LULU Kafungwa jela miaka miwili, Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba ameishukuru mahakama kwa kutenda haki, na ameenda kulia makaburini alikozikwa mwanaye.
Mama wa Muigizaji Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amefunguka na kusema kwamba leo atakwenda makaburi ya kinondonni alipoziikwa mwanaye ili kwenda kumzika upya. Mama Kanumba Mama Kanumba ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kumhukumu kifungo cha miaka miwili Muigizaji Elizabeth Michael ambaye alikuwa mtuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia yaliyopelekea kifo cha muigizaji huyo.”Kwa sasa sina la kusema ila naishukuru sana Mahakama kwa kutenda haki, pia niishukuru sana Serikali yangu lakini pia nikitoka hapa nitakwenda makaburini kwa ajili ya kumzika upya mwanangu Kanumba”.
Mama Kanumba Kwa upande wa Wakili wa Muigizaji Lulu Peter Kibatala ameweka wazi kwamba watakata rufaa kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa mteja wake. Muigizaji Lulu leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua muigizaji mwenzake ambaye pia alikuwa mpenzi wake Steven Kanumba usiku wa Aprili 7 2012.
Unadhani ni haki kwa Lulu kufungwa miaka miwili ikiwa Kanumba ndiyo harudi tena???
Source : Breaking News Tanzania