Kala Jeremiah Kuwania Urais Tanzania

download

Msanii Kala Jeremiah ambaye amekuwa kifanya muziki wenye kuhamasisha sana jamii, amesema iwapo ataingia kwenye siasa ataingia kwa lengo la kuwa Rais wa nchi, na sio nafasi nyingine.

Kala ametoa kuli hiyo  alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha 5SELEKT kinachorushwa na East Africa Television, na kusema kwamba nafasi ya hiyo ya urais ambayo ndiyo nyadhifa kubwa serikalini, ndiyo anayoikusudia kwenye maisha yake, kwani kama ni ubunge ameshafanya sana kazi za ubunge.

“Wengi wananishauri niingie kwenye siasa, unajua kauli ya wengi ni kauli ya Mungu, kama nitaamua kuingia kwenye siasa nafasi ya urais ndo itanifaa zaidi kwa sababu ubunge nishafanya, nilipotoa wimbo na dada yangu Nakaaya wengi walikuwa wananiita mbunge, hivyo siwezi kuingia kwenye siasa kwa kutamani kuwa mbunge, nitatamani kuwa Rais”, amesema Kala.Mara ya mwisho Kala alitoa wimbo unaoitwa ‘wana ndoto’ na kumpatia mafanikio makubwa kwa kupewa tuzo maalum, na hivi sasa ameachia wimbo wake mpya unaoitwa ‘Kijana’.

Vibe Download Button

Leave a Reply