Diamond Platnumz Ft Rayvanny ~ Iyena | Lyrics

download

AAh Leo Chereko chereko
Mwanenu nimekuwa
Zile kuringa mideko itapungua
Asante mama ulinifunza nkajua
Baba kasema kuomba mwiko
Raha ya chumvi kununua
Tena si kwa nazi
Si hirizi za waganga
Kwa baraka za baba na mama Tu na dua
Waambie paparazi
Pingamizi wenye viranga
Waliosema hayawi hayawi yamekuwa
Ooooh OO

[CHORUS]
Iyena Iyena, Iyena Iyena
Iyena Iyena, Kwaheri tutaonana
Iyena Iyena, Iyena Iyena (Aah Iyeena)
Iyena Iyena, Ntawakumbuka sana

Ooh! Ndoa baraka
Ukipata ushukuru
Maana wanayoililia ni wengi sana
Kwetu talaka
Kuitoa ni kufuru
Nimefunzwa vumilia
Niushinde ujana
Ili kesho mahususi
Kusudi wasinong’one
Embu nichumu niringe washushuke
Na hii pete ya harusi
Nakuvisha waone
Wakale sumu
Wavimbe wapasuke

Eeh!
Ati nashika nanga
Nteke nsichomoke ndani
(Anameremeta)
Futa namba wablock vimada wa zamani
(Anameremeta)
Sio vijembe vya kanga waziwazi
mambo hadharani (Anameremeta)
Waliopanga mwenye nyumba kaja
ndani (Anameremeta)

[CHORUS]
Iyena Iyena (Aah iyoyo), Iyena Iyena
(Aah Eeeh)
Iyena Iyena, Kwaheri tutaonana
(Oh! Kwaheri Baba Mama)
Iyena Iyena (Iyeeena), Iyena Iyena
(Aah Eeh)
Iyena Iyena, Ntawakumbuka sana

[RAYVANNY]
Imefika tamati, Tulisubiri kitambo
Leo samaki, Kanasa kwenye chambo
Pongezi kwa kamati
Yanavutia mapambo
Napata picha safi
Litanikoma bundle
Mwanamke usafi
Gaga kulisugua
Mume akirudi sharti
Viatu kumvua
Kitandani marashi
Massage kumchua
Kisha anza sayansi
Viuno kutengua
Mambo ya kuzima taa
Si mahaba ni kuwanga
Washa japo ka mshumaa
Mumeo aone shanga

Eeeeh!
Makeup kinanda
Kaka suit kama mbunge
(Anameremeta)
Mulo changa muda kujipooza na punje
(Anameremeta)
Momo ndani Shivo amekuja na
Fumbwe (Anameremeta)
Kula chanda ukishiba ruksa kafunge
(Anameremeta)

[CHORUS]
Iyena Iyena (Aah iyeee), Iyena Iyena
(Aah iyoyo)
Iyena Iyena, Kwaheri tutaonana
(Eh Kwaheri Baba Mama)
Iyena Iyena, Iyena Iyena
Iyena Iyena, Ntawakumbuka sana

Saa nataka kusasambua (Sasambu)
Me nasasambua (Sasambu)
Aby Dad nasasambua mimi (Sasambu)
Sasambua Tuone
Mguu moja juu (Sasambu)
Usishushe chini (Sasambu)
Cheza jitazame (Sasambu)
Sasambua Tuone

Aisha kimobitel (Sasambu)
Nipe za baloteli (Sasambu)
Nyonga kibaiskeli (Sasambu)
Sasambua, Tuone

Akaa kama unashika ukuta (Sasambu)
Ifanye unashusha (Sasambu)
Taratibu zungusha (Sasambu)
Sasambua  Tuone
Sasambu! Sasambu! Sasambu!
Sasambua Tuone

Kama unawasha bajaji (Sasambu)
Imwagie na maji (Sasambu)
Tuwakomeshe vizazi (Sasambu)
Sasambua Tuone

Leaving A Comment and Sharing This Post With Your Friends,You Stand A Chance To Win $5 Worth of Airtime TODAY!

download Nyimbo mpya