Bifu Ndogo : NASSIZU Murume Amchana ALIKIBA

download

NASSIZU  Amchana ALIKIBA Kwenye Wimbo Wake Mpya.

Msanii chipukizi wa humu nchini NASSIZU MURUME ambaye anatokea pande za Meru, ameachia kazi mpya inayokwenda kwa jina ‘Ngoja Baadaye’, mle ndani amewachana wanasiasa na wasanii haswa msanii wa bongo flava ALIKIBA.

Nassizu anadai kwamba walipokutana na mkali huyo wa hit song ya ‘Seduce Me’ kwenye kipindi cha CHURCHILL SHOW, ALIKIBA alimuahidi watafanya kazi ila kila anapompigia simu KIBA anamuambia angoje baadaye, hadi ikafika kipindi NASSIZU akamuuliza KIBA anataka hela ngapi ili wafanye kazi.

Kwa upande wangu naweza kumuelewa ALIKIBA, kila msanii huwa na mipango yake wakati mwingine anakua na plan na strategy ya mwaka nzima, tena kufanya collabo ni hiari yake, isitoshe KIBA anaweza kukubali kufanya kazi na NASSIZU lakini asipoiskuma vizuri huenda kazi hiyo isifanye vizuri. Ni vyema afanye kwa hiari yake ndio pia aweze kuiskuma vizuri hadi Tanzania. Kitu kingine KIBA tayari ni mmoja wa Wasanii wa Bongo Flava Wanaopendwa sana Kenya, tayari ashateka hii market, so sidhani kama msanii kama NASSIZU anaweza kumuongezea mashabiki maana tayari ana fanbase kubwa, wasanii wengi hufanya collabo ili kubadilishana mashabiki na kuongeza umaarufu.

Kingine cha mwisho NASSIZU angefaa awe na subira ama ajipange vizuri, kihela na ngoma nzuri aeleke Tanzania kumtafuta KIBA waketi chini wazungumze huenda pengine angemuelewa zaidi maana face to face discussion huwa much better kuliko kuongea na simu, all in all hayo ni maoni yangu, Wewe ongezea yako baada ila kwanza sikiliza nyimbo hii ya NASSIZU MURUME.

By Sameer Bry

download Nyimbo mpya