#AbyDad Achomoa Kuvujisha Ngoma Ya
#Alikiba na #Patoranking
Producer Aby Dad amekanusha taarifa za kuvujisha kolabo ya Alikiba na Patoranking kutoka nchini Nigeria. Kwa siku za hivi karibuni wimbo huo umekuwa ukisambaa mtandaoni na Alikiba alipoulizwa alikiri uwepo wa kolabo hiyo lakini kitendo cha kuvunja ni kitu kilichomshangaza kwani ilikuwepo studio na muda wake wa kutoka ulikuwa bado.
Akizungumza na E-Newz ya EATV Aby Dad amesema asingeweza kufanya kitendo hicho kwani yeye ni mfanyabiashara na kuongeza kuwa kufanya hivyo kungeua biashara yake.“Hicho kitu kitaniharibia biashara kwa sababu watu wataogopa kuja kwangu kufanya bishara, kuvujisha wimbo wa msanii ni tatizo kubwa sana na hasara kutokana nyimbo ya msanii inapovuja halafu kukawa na mteja mwingine anataka kufanya kazi na wewe ataogopa kwa sababu tabia yako ni kuvujisha nyimbo za watu,” alisema Aby Dad.
Hata hivyo alisema asingependa kuongelea suala hilo kiundani kuni kuna mambo yaliyojificha nyuma ya pazia ikiwemo kutolipiwa kolabo hiyo na kuna haki zake anadai kutoka kwa msanii huyo. Bongo5/Peter Akaro –